JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
OFISI YA MKUU WA MKOA WA DODOMA
MTIHANI WA UTAMILIFU(MOCK) YA AWALI YA MKOA
DARASA LA SABA, 19
NOVEMBA, 2015
1. Soma
maelekezo yote yaliyotolewa kwa umakini.
2. Andika
jina lako, Wilaya, Shule na somo kwa
usahihi katika karatasi yako ya kujibia.
3. Jibu
maswali yote katika kila sehemu.
4. Andika
herufi ya jibu sahihi kwa kila swali katika karatasi yako ya kujibia uliyopewa.
5. Simu
za mkononi haziruhusiwi ndani ya
chumba cha mtihani
Chagua
jibu lililosahihi na uandike herufi inayohusika mbele ya namba ya kila swali
katika karatasi yako ya kujibia uliyopewa
1. Katiba
yaTanzania inayofanyiwa Marekebisho sasa ni ya mwaka
a) 1961
b) 1965
c) 1964
d) 1977
e) 1967
2. Serikali
ya kijiji au mtaa imeundwa chini ya sheria ya __
a) Serikali
kuu
b) Bunge
c) Baraza
la mawaziri
d) Mahakama
kuu
e) Serikali za
mitaa
3. Waziri
mkuu akishateuliwa na Rais lazima athibitishwe na
_____________
a) Mahakama
b) Usalama
wa Taifa
c) Baraza
la mawaziri
d) Bunge
e) Spika
wa bunge
4. Katika
nchi mhimili wenye mamlaka
ya kuongoza na kuendesha nchi ni ..............
a) Jeshi
la Polisi
b) Bunge
c) Serikali
d) Mahakama
e e) Magereza
5. Mwenyekiti wa
Kamati ya ulinzi na usalama
wa Mkoa ni
a) Mkuu
wa Wilaya
b) Katibu tawala
wa Mkoa
c) Afisa utumishi
wa Mkoa
d) Mkuu wa Mkoa
e) Kamanda wa Polisi
wa Mkoa
6. Chombo
chenye wajibu wa kulinda amani na usalama wa Taifa ni _________
a) Kila
raia
b) Jeshi la
wananchi
c) Polisi
d) Usalama
wa Taifa
e) Mahakama
7. Umuhimu
wa utamaduni katika jamii zetu za kitanzania
ni ___
a) Kuitambulisha
jamii
b) Kuleta
michezo ya asili
c) Kuzuia
maendeleo
d) Kugawa
wananchi kwa kutumia ukabila
e) Kuburudisha
jamii
8. Kati
ya zifuatazo ipi ni mila potofu katika jamii zetu ____
a) Kupatiwa
elimu
b) Kulindwa
c) Ukeketaji
d) Ngoma
e) Maziko
9. Chombo
chenye wajibu wa kusimamia masuala ya fedha nchini Tanzania ni____________
a) VICOBA
b) Benki
ya wananchi (NMB)
c) Wizara
ya fedha
d) SACCOS
e) Benki kuu ya
Tanzania (BOT)
10. Uchumi
wa taifa la Tanzania hutegemea
zaidi ________
a) Biashara
b) Misitu
c) Kilimo
d) Viwanda
e) Madini.
11. Uchaguzi
mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu utakuwa ni uchaguzi wa ngapi tangu kuanzishwa mfumo wa vyama vingi nchini
Tanzania ___
a) 3
b) 4
c) 6
d) 5
e) 6
12. Tanzania
inaongozwa kwa mfumo wa aina ya _
a) Kiimla
b) Kimapinduzi
c) Kidemokrasia
d) Kibepari
e) Kikabaila
13. Shirika
la umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi ni ____
a) UNHCR
b) WHO
c) UNICEF
d) UNIDO
e) HABITAT
14. Ni
nchi ipi kati ya zifuatazo si mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
a) Tanzania
b) Kenya
c) Zambia
d) Uganda
e) Rwanda
15. Katibu
Mkuu wa sasa wa Umoja wa Mataifa anaitwa
a) Barrack
Obama
b) Asha
Rose Migiro
c) Koffi
Anan
d) Ban Ki –Moon
e) Hillary
Clinton
16. Waziri
Mkuu wa
kwanza wa Tanzania alikuwa
a) Mwl J.K Nyerere
b) Edward Moringe
Sokoine
c) Rashidi Mfaume
Kawawa
d) Salim
Ahmed Salim
e) Joseph Sinde
Warioba
17. Kiongozi
ambaye huteuliwa na Rais na kuapishwa na
mkuu wa mkoa ni ___
a) Mkuu wa wilaya
b) Katibu
Tawala wa Wilaya
c) Kamanda
wa Polisi wa Wilaya
d) Mkurugenzi
wa Wilaya
e) Wabunge
18. Chombo
chenye wajibu wa kusimamia haki za wananchi ni____________
a) Bunge
b) Katiba
c) Mahakama
d) Serikali
za mitaa
e) Vyama
vya siasa