OFISI YA WAZIRI MKUU
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
OFISI YA MKUU WA MKOA WA DODOMA
MTIHANI WA UTAMILIFU(MOCK) YA AWALI YA MKOA
DARASA LA SABA, 2016
SOMO HISTORIA
MUDA: SAA 1:30 (4:30 – 6: 00 MCHANA)
19 NOVEMBA, 2015
1. Soma maelekezo yote yaliyotolewa kwa umakini.
2. Andika jina lako, Wilaya, Shule na somo kwa usahihi katika karatasi yako ya
kujibia.
3. Jibu maswali yote katika kila sehemu.
4. Andika herufi ya jibu sahihi kwa kila swali katika karatasi yako ya kujibia uliyopewa.
5. Simu za mkononi haziruhusiwi ndani ya chumba cha mtihani
1. Gavana wa mwisho wa kiingereza hapa Tanganyika alikuwa ____________
a) Sir. Donald Cameron
b) Sir Horacce Byatt
c) Carl Peters
d) Julius von Sodden
e) Sir Richard Turnbull
2. Sultani wa kwanza kuitawala Zanzibar aliitwa.....
a) Seyyid Said
b) Said Bargharash
c) Sultani Bin Jamshidi
d) Saidi Majid
e) Said Salum
3. Uchumi wa Kikoloni katika Tanganyika na Zanzibar ulihakikisha upatikanaji endelevu wa
a) Mahitaji
b) Malighafi
c) Watumwa
d) Elimu
e) Huduma
4. Azimio la Arusha lilitangazwa huko Arusha mwaka..............
a) 1961
b) 1962
c) 1964
d) 1967
e) 1977
5. Msingi mkuu wa uchumi wakati wa mfumo wa Ukabaila ni ____
a) Fedha
b) Ardhi
c) Binadamu
d) Utumwa
e) Mtaji
6. Lengo kuu la wakoloni kutawala Tanganyika na Zanzibar ilikuwa ni............
a) Kujenga viwanda vikubwa kama vya ulaya
b) Kuzalisha malighafi kwa gharama ndogo
c) Kuendeleza jamii za Tanganyika na Zanzibar
d) Kuleta malighafi bora kutoka Ulaya
e) Kuanzisha mashamba makubwa
7. Vyama vya TANU na ASP viliungana rasmi mnamo ……….
a) Tarehe 5 february, 1977
b) Tarehe 8 february, 1977
c) Tarehe 12 january, 1964
d) Tarehe 26 Aprili 1964
e) Tarehe 5 July,1977
8. Gavana aliyeanzisha Baraza la kutunga sheria nchini Tanganyika aliitwa ...........
a) Richard Turnbul
b) Donald Cameroon
c) Edward Twinning
d) Horrace Byatt
e) John Scolt
9. Chifu Mangungo wa Msovero alisaini mkataba wa ulaghai na wakala wa Kiingereza aliyeitwa ----
a) Horace Byatty
b) Karl Peters
c) Julius Von Sodden
d) Willium Macknon e) Zelewisky
10. Mlinzi wa mali na familia katika jamii ya kimasai aliitwa____
a) Mtwa
b) Laiboni
c) Morani
d) Layoni
e) Mtemi
11. Mfumo wa Uongozi unaofuata misingi ya haki na sheria ni _____
a) Utawala wa kiimla
b) Utawala wa kisheria
c) Utawala bora
d) Utawala wa kidemokrasia
e) Utawala juu ya sheria
12. Taifa lililokomesha biashara ya utumwa katika Afrika Mashariki ni -------
a) Wajerumani
b) Wafaransa
c) Wareno
d) Waingereza
e) Waarabu
13. Mkutano wa kuligawa Bara la Afrika ulifanyika kati ya Mwaka
a) 1884 na 1885
b) 1886 na 1890
c) 1886 na 1888
d) 1845 na 1813
e) 1984 na 1985
14. Ngome ya Yesu (Forty Jesus) iliyojengwa na Wareno ilikuwa katika mji wa ___
a) Kilwa
b) Mombasa
c) Kalenga
d) Nairobi
e) Malindi
15. Wajerumani walijenga reli ya kati maeneo ya Pwani na Bara mnamo mwaka
a) 1897
b) 1900
c) 1905
d) 1960
e) 1805
16. Ni nchi ipi kati ya hizi haikutawaliwa na wakoloni?........
a) Angola
b) Tanzania
c) Ghana
d) Ethiopia
e) Zimbwabwe
17. Wakoloni wa kwanza kuitawala Tanganyika walikuwa __
a) Wereno
b) Wabeligiji
c) Waingereza
d)